Inter Region Economic Network, Nairobi, Kenya  

Home
About IREN
Media & Press
Projects
News & Newsletters
Articles
Events
Resources
Speeches and Publications
Student Outreach
Contact IREN

Chapter 31 - SURA YA THELATHINI NA MOJA


MASHTAKA

Walipomwona kiongozi wao, George, akielekeakwenye mlango,wale wanaume wengine pale pambizoni walichukua mikoba yao na kufuata nyuma karibu

"Nambari mbili,"akasema George, "hebu nielezee tena lile tatizo la hatia,tafadhali,"George alitaka kumwonyesha Jonathan jinsi wanasheria wake walivyokuwa wajuzi.

Kundi zima lilitembea harakaharaka kuelekea upande wa chini wa ule ukumbi,huku mikono ya George ikiwa bado kwenye shingo ya Nambari Mbili na Jonathan. "Unajua,"alisema Nambari Mbili, "kile kipande cha chuma chaweza kungoka kwenye kijiti na kumgonga labda mtu aliyesimama kando kwa hivyo sharti tukilinde pamoja na wawekezaji wengine."

"Kunilinda mimi wakati kipande cha chuma kikimgonga mtu mwingine? Unamaanisha nini hasa?" alisema George,akimlisha maswali huyo mwanasheria

"Huyo majeruhi aweza kukufungulia mashtaka mahakamani kujaribu kukushurutisha ulipie uharibifu - tija aliyoipoteza, athari ya kisaikolojia, ada ya kisheria, na kadhalika." Lile kundi halikujizuia kumkanyaga visigino Jonathan likijitahidi kumfuata George unyo unyo. Kwa waenda-kwa-magoti, ama kweli kasi hiyo ilikuwa ngumu sana, lakini walijifariji kwa wazo kuwa wangepata marupurupu ya ushuru mwishoni mwa mwaka.
"Mashtaka yaweza kunivuruga kabisa!" alisema George kwa uoga wa kujitia huku akimtizama jicho la kiupembe Jonathan kupima hisia zake.

Nambari Mbili aliendelea bila kufahamu kuwa alikuwa akielekezwa. "Kwa hivyo maarifa mapya maalum yametiwa na Baraza la Watawala ili usihusishwe na hasara wanazozipata wengine".
"Maarifa mengine mapya? Ni nani anayemiliki hati-kiritimba yayo?" akauliza Jonathan kwa ukembe.
Nambari Mbili alielekea kukanganyika, kisha akaendelea huku akilipuuza swali la Jonathan. "Huwa twaweka hizi fomu kwenye jalada na kutia herufi 'Lpr' baada ya jina la kampuni yako". Bila kukosea hata hatua moja, Nambari Mbili alijitahidi kulifungua shanta kutoa kitopa cha karatasi. "Hiyo inanikumbusha bwana Selden, tafadhali tia saini kwenye mstari hapo chini".
Jonathan alivutiwa, "Lpr ni nini?" akauliza huku akijikwaa kidogo na kujirekebisha.

"Lpr. Inamaanisha 'Limited personal responsibility' akasema Nambari Mbili. Bwana Selden akiisajili kampuni yake hasara kubwa kabisa anayoweza kupata katika mashtaka ni pesa alizotumia kuwekeza. Mali yake yaliyosalia yatakuwa salama dhidi ya wahanga.
Ni namna fulani ya bima ambayo Baraza humuuzia mtu kwa kumtoza ushuru fulani wa ziada. Kwa sababu Baraza hujaribu kuzuia hatari ya hasara ya pesa, watu wengi watawekeza kwenye kampuni yetu. Na hawatafuatilia sana tunachofanya."
"Mambo yakiwa mabaya kabisa ,"akatoa kauli George," "Twaweza kufunga kampuni na kujiendea zetu.Kisha tuanzishe nyigine kwa jina tofauti . Werevu huo, eh?"

Hapo, jicho lake George lilikumbana na mwanamke mbichi wa kupendeza sana aliyekuwa akija upande huu wa ukumbi . Alikuwa akitembea kwa mwendo wa kupindapinda zaidi ya inavyokubalika kisheria kwenye barabara ya umma. Alienda kwa namna ya kusisitiza kila mpindo .Alipokuwa akigeuka kumtizama yule mwanamke akipita ,George alijikwaa akaanguka ghafla huku akijigonga vidole vyake vilivyotunzwa vizuri ukutani. "Ooh !" alilia kwa uchungu,huku akitupa mikono na miguu yake kila upande. Alijaribu kujiinua kutokasakafuni huku akiyalalamikia maumivu makali mkononi mwake na kwenye sehemu ya chini ya mgongo . Mawakili zake walimzunguka kwa fujo huku wakitupiana maneno makali.Wachache walisaidia kukusanya vitu vilivyotawanyika kutoka mifukoni mwa George , wakati wengine wakijitahidi kuandikaandika na kuchora picha za pale pahali.

"Nitawasilisha mashtaka!" akanguruma George huku akishikilia vidole vyake vilivyochubuka na vyenye damu kwenye kijitambaa chake laini. "Nitamsagasaga huyo mjinga anayehusika na hiki kizingiti kwenye sakafu! Na wewe binti , nitakutana nawe mahakamani kwa kunitatizia makini yangu kwenye shughuli zangu!" Kwa haraka ya mmuliko wa mwanga, mawakili kadhaa walimkimbilia yule mwanamke , kumuomba jina na anwani yake.

Kwa kustaajabu, yule mwanamke alinguruma kwa kiburi "Kunishtaki? Unajua mimi ni nani?"
"Hainijlishi,"akasema George kwa mwako. "Ukiwa mkubwa zaidi ndiyo bora .Nitakushtaki!"
Huku akitetemeka na kujitahidi kuzuia ghadhabu yake , mwanamke alijibu , "Huwezi kufanya hivyo, hata! Mpenzi wangu ,Carlo, yaani Carlo Ponzi," aliridia ili kisisitiza , "Yuasema kuwa urembo wangu humfaidi kila mtu -kwamba ni wa manufaa kwa uma mzima. Ndivyo alivyoamua -aliniambia usiku wa jana!" Bila kuwazia alitia mkono kwenye kibogoho akatoa kioo. Alichoona kilimuudhi. Pambo lake la macho lilionekana kana kwamba kakandikwa tu. "Sasa hebu ona ulichoyafanyia manufaaya umma!Carlo anasema kuwa kila mtu anafaa kulipia bidhaa za umma. Daima hutia vipodozi vyangu kwenye makadirio yake ya matumizi ya fedha .Lazima utajuta ! Ushuru wako utakwenda juu kwa sababu hii!" Alikifutika kioo chake kwenye kibogosho na kujiendea hamsini zake kutafuta chumba cha poda.

Kwa kumhurumia yule mwnamke kwa kiasi fulani,Jonathan alisaili "Ni kweli utamshtaki mahakamani? Kosa lake hasa ni lipi?"

Akimpuuza Jonathan, George alitambaa kwenye sakafu akisaka kilima chochote, ushahidi wa kuzembea kwa mtu fulani katika wajibu wake. Alisita bada ya kukiona kishimo na akapiga kite, "Ndicho kilichobabisha, Nambari Mbili!chungua ni nani anayehusika. Nitampoka kazi yake na kila peni analomiliki. Na jina la yule mwanamke ni nani?

"Tulizana ,George ," akasema Nambari Mbili. "Huyo ni msichana wake Ponzi. Sahau mambo yake ukitaka kuifanyia marekebisho sheria ya wafanyakazi wa misitu.Hata hivyo hili jengo ni mali ya ikilu. Kwa idhini ya Watawala ,twaweza kuwatilia mashtaka walipa ushuru."

George alitia tabasamu pana na kupaaza sauti, "Nambari Mbili, wewe ni staid mkubwa. Tia hilo kwenye ajenda ya Tweed !Ama kweli ,Watawala hawajali chochote toka mifukoni mwao. Hata tutahakikisha wanapata sehemu yazo."Alijaribu kukijia ukubwa wa kiasi ambacho Bi Tweed angeng'oa kutoka kwake kwa ajili ya upendeleo huo. Maumivu ya George yalikuwa yakiishia haraka haraka. "Hili linanipa fursa kwenu mfuko weye kia krefu kulikoyote."

"Utawaagiza Watawala kufidia kujeruhiwa kwako?" akauliza Jonathan.

"La ,mpumbavu wewe ," akatoka George. "Watawala wana Lpr kamili .La ,Watanipa hao walipa ushuru kwa urahisi sana . Shabash ! nitakusanya kisawasawa."






© Copyright 2005,
Inter Region Economic Network, Nairobi, Kenya, All Rights Reserved.