Chapter 32 - SURA YA THELATHINI NA MBILI
MATIBABU POTOVU
Jonathan aliufuata msafara wa George hadi nje ya Ikulu ya Watawala kwenda kutafuta msaada wa kimatibabu. Upande ule mwingine wa Ikulu jengo refu jeupe lilichukua sehemu kubwa ya ule mfululizo wa majengo. Lile kundi liliingilia kwenye mlango uliokuwa karibu kabisa .Ghafla kilio cha maumivu kilitokea kwenye dirisha lililokuwa wazi kwenye sehemu ya katikati mwa jengo hilo. Jonathan alikimbia na kulifikia dirisha hilo wakati tu vifungio vyake vikianza kujifunga. Aliruka na kukinyaka kimojawapo cha vifunguo hivyo, akikishikilia wazi.
"Toka hapo ," akamtokea mwanamke mmoja wa tambo aliyekuwa ndani .Uso wake mwekndu wenye hasira ulikuwa kinyume na sare yake nyeupe iliyomfunika kutoka utosi hadi wayo.
"Ni nini kinachoendelea huku?" akashikilia Jonathan. "Mayowe ni ya nini?"
"Hayo hayakuhusu chochote . Haya ondoka sasa!"
Kwa mastaajabu ,Jonathan alishikilia kwa nguvu zaidi. "Siondoki hadi unieleze unachofanya!Unamwumiza mtu!"
"Naam, ama kweli tunamwumiza mtu," akasema yule mwanamke. "Ni njia ipi nyingine ya kuwaponya ? Niamini mimi ni daktari."
Kwa hakika kabisa, Jonathan aliliona jina na anwani ya yule mwanamke likiwa limeshonwa kwenye sare yake-Dict. Aigail Flexner.Jonathan alilipuka "Mnawaumiza watu ili kuwaponya? Mbona msiachane tu nao?
"Sharti tuwauwe pepo .Wakati mwingine ni vigumu kuhakikisha kuwa mgonjwa haumi? Wakati huo" akapasua daktari kama ukweli usiopingika. Alivyokuwa ameudhika usumbufu wa Joathan alitizama huku na huku kuonakama angepata usaidizi kumuondolea mbal huyu kijana fidhuli "Oh, sawa," alisema akionyesha kulegea. "Nitakuhakikishia kuwa tunawasaidia watu! Zunguka wa mlango wa ando a nitatembeza kidogo kwa ziana ya kimafunzo."
Huku akishuku ,jonathan aliishia kukiwachilia kifungo na kwenda alikoambiwa. George na wenzake walikuwa wamepita mlango huo huo lakini Jonathan hakuona dalili yote yao mle ndani. Alikuwa kaingia kwenye chumba kilichojaa watu wa kila umri, wengine wamekaa na wengie wamesimama bega kwa bega kwenye kuta.Baadhi waliomboleza kwa sauti huku wakinyosha mikono na miguu iliyozungushiwa bendeji na kufungwa vitata. Baadhi walinung'unika, waliranda kwa shauku, au waliwafariji wapendwa wao. Wengi walikuwa na malazi na vyombo vya kupikia vikiwa vimerundika kando yao, ishara kuwa wamekuwa pale kwa kipindi kirefu. Jonathan alishindwa kuelewa muda waliohitajika kuongoja watu hawa.
Dkt Flexner aliufungua mlango wa ndani na akamfanyia ishara ya mkono kumwita Jonathan. Ule umati ulinyamaza na kutulia kimya ;walimtazama Jonathan kwa inda alipokuwa akipita mbele yao.Daktari alimwingiza kwenye chumba kimoja kisicho madirisha, kilichojaa madawati, makarani na rundo la karatasi zilizopangwa darini.Alimwongoza hadi kwenye mlango mwengine , ulioelekea kwenye kieneo kidogo cha duara kilichozunguka na roshani yenye viti. Harufu nzito ya kemikali na uozo ilizishambulia hisia za Jonathan.
Watazamaji kadhaa walikiegemea chuma cha roshani. Pale chini wanaume na wanawake kadhaa waliovalia mavazi meupe,yamkini madaktari na wauguzi, walisongamana kwa makini kumzunguka mgonjwa mmoja mnene aliyekuwa kafungwa kwenye meza fupi.
"Ili kumponya huyu mgonjwa," alinong'oneza yule daktari kwa huzuni , "Madaktari wenye imani wanakata mishipa yake na kuifugua ili pepo waweze kuvuja pamoja na damu. Mara moja moja huwa twawatumia rua." Aliashiria meza moja iliyokuwa kando ya mgonjwa .Meza hiyo ilibeba namna mbali mbali za visu , misumeno ,mihuma , na chupa za maki na maumbo mbali mbali. Ruba wenye miili ya kuteleza, maki ya kidole gumba cha binadamu , walivinginya huku wakimwagikia kando ya bakuli la chuma.Jonathan aliihisi tumbo yake ikipinduka.
"Tusipofaulu hivyo, kina mama na wanaume wetu wa Sayansi hutumia kemikali kuwasumu pepo hao. Tunahiari kutumia aseniki, wanja wa manga, na vifanyizo vya zebaki .Hatua kubwa ilioje tuliyopiga kwenye Sayansi ya Matiabu! Ninakwambia,karne nzima baadaye matibabu wataustaaabia ufanisi wetu."
"Si hizo sumu zaweza kuua?" akasema Jonathan. Alikumbuka kuwa mjombake akiuza michanganyiko kama hivyo vifanyizo vya kutumiwa kuwaua panya kule nyumbani. Alikumbuka kwa kiasi fulani alivyowasikia wazee wakizungumzia vitu hatari vya namna ile vilivyotumiwa kwa matibabu hapo zamani. Lakini si mambo ya namna ile yaliisha kitambo kile?
"Hakuna njia nyingine ," akasema yule mwanamke daktari kwa namna ya kutia moyo. "Kukata, kuchora na umu ndiyo matibabu pekee yalivyo salama na ya kutegemewa."
"Na njia hiyo hufaulu katika kila tukio?"
"Matiabu hayo hufaulu kuwafutilia mbali pepo asilimia mia moja ya wakati husika! na," alihemka, kiwango cha kustaajabisha cha kupoa cha asilimia ishirini na saba.
Jonathan alikodoa macho . Mmoja wa wale matabibu aliichana tumbo ya yule mgonjwa na damu ikaanza kuchuruzika. "Anaugua ugonjwa upi?"
"Opsonin rot of the nuciform sac," akajibu Dkt Flexner. "Tuna hakika."
"Hapana njia nyingine yoyote ya kumtibu?"
"Ah!" akamaka. "Wengine wanadai vingine. Inshallah hao matabibu bandia hawapewi vibali vya kutoa tiba. Haitoshi tu kuthibitisha ubora wa matabibu wetu wenyewe ili watu wateue. Ni sharti tuwaharamishe walaghai wanaosingizia kuponya kwa kutumia dawa zisizoidhinishwa mmlo wa kipunzi,kuvu, mimea, pini, mguso, maombi, hewa safi ,mazoezi , na hata wakati mwingine ,haiaminiki." Akakunja uso, "Kicheko ! Tukiwashika tunawatupa korokoroni na kutupilia mali funguo!"
"Na hizo tiba huponya?" akauliza Jonathan kwa upole. "Mh! Zikiponya ni kibahati tu," akajibu. Jonathan aliona jinsi uso wake ulivyoumka. Pua yake ilyogeuka na kuwa nyekundu, ndivyo iliyokuwa na rangi ya kjivu, kama anga iliyotanda mawingu. Pumzi zake zingeweza kuua.
"Na je , itakuwaje mgonjwa akiamua kutumia hizo njia?" akabisha Jonathan. "Ni maisha ya nani kwani?"
"Sawa hasa!" akamaka. Jonathan alikuwa kazindua mada iliyompendeza. Daktari huyo alimvuta Jonathan kutoka kwenye chuma cha roshani na akapitanisha mikono yake minene kwenye kifua chake huku mkoo mmoja akiutia kwenye kidevu.Huku akizungumza kwa makini , alisema, "Ni maisha ya nani? Baadhi ya hawa wagonjwa wenye ubinafsi hudhaniwa kuwa maisha ni yao wenyewe! Wanasahau kuwa maisha yamtu huwa ni ya wengine wote. Sote tunajenga msururu mmoja usioatika kutoka kwa mababu hadi vizazi, sote tukiwa tumeungwa kwenye jumla pana. Kwa manufaa ya jamii ,wataalamu wenye ujuzi sharti wawalinde wagonjwa dhidi ya uamuzi wao usiofaa. Hebu fikiria !Baadhi ya wagonjwa wanataka ama kweli kujiua! Sisi huwa tayari zaidi kuamua lini na vipi watakavyotibiwa."
Alisita kukumbuka jambo kisha akaendelea, "Licha ya hivyo, Baraza la Watawala hulipa kwa ukarimu gharama zote za Matibabu hapa Kisiwani. Wafanya kazi wenye siha wana wajibu kwenye mstari wa ushuru, wajibu ambao unapendekezwa kupitia uamuzi wa Baraza kuhusu uwezo. Wagonjwa wana wajibu kwenye mstari wa kungojea. Wajibu unaopendekezwa kupitia uamuzi wa uhitaji. Hiyo mistari miwili ni sharti siku moja ilingane, kwa hivyo hatuwezi kuwaacha wagonjwa watie dosari ,tena kubwa sana, katika jambo linalohusisha pesa za watu"
Kilio cha uchungu kilisikika tena mle chumani na damu ikazidi kuchuruzika kwenye beseni ilivyokuwa pale sakafuni. Wahudumu walipokea amri na kuzifuata. Daktari mpasuaji alipokezwa vifaa na sifongo zaidi.Huku akiwa amesimama kando yake Jonathan, yule daktari mwanamke alionyesha imani usoni mwake. "Ninayahisi maumivu yake," akanong'ona.
"Mtu hupataje kibali ,"alisaili Jonathan, "ndipo akaweza kuwafanyia watu huu uamuzi wa kufa au kuendelea kuishi?"
"Huchukua miaka mingi sana ya matayarishi .Sharti mtu apate mafunzo murua ya matibabu, na kupita mitihani sufufu. Kama ilivyoidhinishwa na rafiki zetu katika Baraza la Watawala, tulifunga moja wapo ya vyuo viwili vya matibabu kisiwani Korumpo ili kuhifadhi viwango vya juu vifaavyo. Miaka mingi ya utafiti wa kisomi pamoja na tamaduni tukufu, ni mambo yanayotupa hivi viwango. Chama karimu cha kuyalinda matibabu yafaayo huwatunza vibali na kuwahakikishia matabibu mishahara inayoenda sambamba na tabaka lao katika jamii."
"Mishahara mikubwa? Akasema Jonathan.
"Hayo yametosha kwa sasa ."Daktari alimtazama Jonathan kwa kero na kumtaka aondoke .Lakini Jonathan alikataa kukoma kuuliza maswali. "Huwa mwajuaje ni daktari yupi mzuri na yupi mbaya?"
"Huwa twajaribu kuhakikisha kuwa hapana uteuzi usiofaa wala makisio yasiyo na maana .Hapana kitu kama daktari mbaya." Akasisitiza . "Madaktari wote wenye vibali wamehitimu sawa. Ama weli huwapo uvumi hatuwezi kuuzuia umbeya kuhusu uzuri na ubaya. Lakini mamlaka yetu juu ya ripoti huhakikisha kuwa umbeya wowote wa namna ile hauna misingi. "Kwa haraka a umeme alimsukuma nje Jonathan nje kwa mlango wa nyuma na akaufunga kwa komeo.
© Copyright 2005,
Inter Region Economic Network, Nairobi, Kenya, All Rights Reserved.