Inter Region Economic Network, Nairobi, Kenya  

Home
About IREN
Media & Press
Projects
News & Newsletters
Articles
Events
Resources
Speeches and Publications
Student Outreach
Contact IREN

Chapter 33 - SURA YA THELATHINI NA TATU


KINYUME

Punde tu alipotoka kwenye lile jengo nusura amkunguwee Mise aliyekuwa kalala akimsubiri huku akiwa na panya mfu miguuni mwake .Huku akimutizama yule panya wa kuchukiza,Jonathan aliwaza, "Ninaweza kukisia ulikomtoa huyu panya, Mise .Shukrani lakini si shukrani." Yule paka wa Manjano alilipuna sikio lake lililokatika, akionyesha kutojali jinsi Jonathan alivyopuuza yule panya mtamu.

Upande ule mwingine wa bara bara ,Jonathan alimwona mwanamke mmoja mwenye vipodozi tele na aliyevalia rinda la rangi nyekudu ya Mwanga ,lililomkaza maungo.Kila mwanamme alipompita pale barabarani, alitabasamu na kujaribu kumtia kwenye mazungumzo. Hakuelekea kuonekana kuwa ni ombaomba.La, Jonathan alifikiri kuna kitu alichokuwa akijaribu kuuza Alipokosa kufaulu katika juhudi zake na mwanamume huyo, aligeuka ghafla kumtafuta mteja mwingine. Jonathan hakuweza kuelewa ikiwa Mtawala Ponzi ameamua huyu mwanamke mrembo awe bidhaa ya umma ,vile vile.

Kisha alimwona mwanamke mwingine aliyevalia kiajabu akielekea kumkabili. Naye pia alikuwa kajipaka rangi nyingi kwenye midomo na kavalia blauzi nyeusi yenye uwazi uliyoonyesha mwanga mkubwa baina ya madodo yake .Sketi yake fupi iliacha nje miguu yake miororo, ishara kuwa hakuwahi kutembea kwa magoti. Aliposimama na kumtazama Jonathan kwa jicho kavu, alishindwa kabisa kupumua .Alikuwa akikaribia kusema kitu, wakati motokaa ya Polisi ilipotokea kwenye kona na kusimama ghafla baina ya wale anawake wawili.
Wanaume kadhaa wenye kuvalia mavazi meusi waliruka kutoka kwenye ile motokaa ,wakawadaka wale wanawake wote wawili. Wakiwa wamekunja nyuso zao, waliwachuna na kuwatupa kwenye motokaa wale wanawake waliokuwa wakipiga nyende na kutupatupa miguu.Kabla ya Jonathan kupata wakati wa kuingilia, wale polisi walifunga milango kwa vishindo, na dereva akaliondoa lile gari kwa fujo. Mmoa wa wale maafisa alibaki nyuma , akiandika kauli fulani kwenye kijitabu alichokitoa mfukoni mwake.

"Tafadhali, bwana ,"akasema Jonathan, "Ningependa kuripoti wizi."

"Hiyo siyo idara yangu," akajibu yule polisi bila hata kuyaondoa macho yake kwenye kile kijitabu.
Jonathan alikwama. Huku akikitazama kidude cha jina chini ya beji ya yule polisi,Jonathan aliuliza , "Idara yako ni ipi,ah, Afisa Stuart?"

"Ukiuka-adili," akasea yule mwanaume.

"Hebu rudia tafadhali"

"Idara ya Ukiuka-adili .Katika idara yetu tunashughulika na utovu wa adili."

"Kusema kweli wizi ni utovu wa adili ." Alipoona hazungumziwi tena ,Jonathan alisaili."Wale wanawake walikamatwa kwa nini?"

Afisa Stuart sasa aliyainua macho yake kutoka kwenye kijitabu na kuona jinsi uso wake Jonathan ulivyoonyesha mastaajabu. "Hungeweza kuelewa kutokana na maradhi yao? Hao wanawake walikuwa na hatia ya maradhi ya kuwapa wanaume ngono ili wapate pesa. Ingekuwa afadhali kabisa iwapo wangebadilishana hiyo ngono na vitu vingine."

"Vitu vingine ? Yaani kivipi? "akauliza Jonathan ambaye sasa hakujali matatizo yake ila alitaka kufahamu zaidi kuhusu wale wanawake. "Ninamaanisha," akasema polisi, huku akisitasita kila neno, "Hao wanawake wangewaburudisha hao wanaume wao baada ya kupokea vyakula, vinywaji, densi na tiketi ya ukumbi badala ya pesa. Ni vizuri zaidi kwa biashara ya jamii na si kinyume cha sheria hata kidogo." Hapo Jonathan alichanganyikiwa zaidi. " Kwa hivyo haifai kabisa kutumia pesa ili kupata ngono?"

"Japo kuna vighairi. Kwa mfano, shughuli hiyo yaweza kulipiwa pesa ikiwa imerekodiwa kwenye video na kuwasilishwa watu wote mjini. Hapo inakuwa tamasha ya umma, sio ya kibinafsi na hivyo inaruhusiwa. Badala ya kukamatwa, washiriki wanaweza kuisha kuwa mabingwa wa kujivuniwa na kujipa mapato kutoka kwa hadhira lengwa."

"Kwa hivyo ni kujipa pesa kutokana na shughuli hasa ya kimapenzi ya kibinafsi ambayo ni kinyume cha adili?" aliuliza Jonathan.

"Kuna vighairi pia katika shughuli za kibinafsi za kifedha, hasa pale ambapo wanawake wanaohusika wanavaa nguo nzuri ikilinganishwa na hao warandarandaji wa barabarani," akasema Afisa Stuart kwa dharau. "Makubaliano ya muda mfupi, ya saa moja au usiku mmmoja, ni haramu. Lakini katika mahusiano ya kudumu mustakabali mzima baina ya mume na mke, pesa zaweza kutumiwa. Kwa hakika, wakati mwingine wazazi huwahimiza watoto wao kufanya makubaliano ya namna hiyo. Wale wanaowania hadhi kamili wametukuzwa hasa kwa sababu ya tabia ya namna hii. Yakifanywa ifaavyo makubaliano kama hayo huwa ni njia halali ya kuboresha hadhi na usalama wa kijamii".

Yule polisi alimaliza shughuli yake ya kuandika na kutia mkono wake kwenye mkoba. Alitoa kijitijiwe na misumari kadhaa, "waweza kunisaidia kidogo hapa?"

"oh naam", akasema Jonathan akionekana kutokuwa na shwari. Alizichukua mbao kadhaa zilizokuwa zimerundikwa kando ya barabara na akamwashiria Jonathan, "Haya, shika upande huu juu. Ninahitaji kuyaziba madirisha ya duka hili".

"Kwa nini unaliziba duka hili?"

"Duka hili limeisha fungwa", akasema kwa sauti iliyotatizwa na misumari aliyoshikilia mdomoni mwake. "Mwenyewe alipatikana na hatia ya kuuza picha chafu na akatiwa korokoroni".

"Picha chafu ndicho nini?" akasaili Jonathan, akionyesha kabisa kutoelewa.

"Aahm, picha chafu ni picha ya kitendo fulani kibovu na kinachoudhi".

"Huyo mwenye duka alikuwa akitenda kitendo cha kuudhi?"

"La yeye alikuwa akiziuza tu picha".

Jonathan alilifikiria hili kwa makini huku yule mwanamme akimalizia kuupigilia msumari ubao wa juu kwenye mlango. 'Kwa hivyo uuzaji wa picha chafu unafanya mtu awe na hatia ya kitendo chenyewe?"

Sasa ilikuwa zamu ya yule polisi kusita ili kutafakari. "Naam, kwa kiasi fulani ni kweli. Watu wanaouza picha kama hizo wana hatia ya kuendeleza kitendo chenyewe. Wanunuzi huathiriwa kwa urahisi, ushafahamu?"
Jonathan alijipiga kipajini kwa kiganja chake. "Ninaelewa sasa! Hii sharti ndiyo afisi ya gazeti. Mmekamata wapiga picha za gazeti kwa sababu walipiga picha za vita na mauaji! Lakini je, magazeti yenu yana hatia ya kuchochea vita na mauaji kwa sababu tu eti yanachapisha na kuuza picha za mambo hayo?"

"La, la mmh!" alimaka afisa, huku akitisa kidole gumba chake na kuachilia mfululizo wa maneno makali ya kulaani. Alikuwa kaukosa msumari na kujigonga kidole gumba. Afisa Stuart alitizama huku na huku kwa makini kuona kama kuna yeyote yamkini kamsikiza akiapa. Huku akikusanya vifaa vyake, alianza tena, "uchafu ni tendo la ngono - hutendwa tu na watu potovu! Watu waungwana hulaani tabia kama hiyo. Kwa upande mwingine", akasema huyo jamaa, "mapigano na mauaji ni mambo ambayo waungwana na wapotovu wote waweza kusoma kuyahusu na kuyafanya pamoja. Kwa hakika, uarifu mzuri wa mambo haya waweza kuwapa waandishi wa habari matuzo". Punde tu baada ya kuupigilia ubao wa mwisho, Afisa Stuart alizichukua zana zake na kujiendea zake.

Jonathan alimtizama paka wake Mise pale chini. "ninadhani ana shughuli nyingi sana zinazohusu utovu wa adili kiasi hawezi kunisaidia katika tatizo langu linalohusu tu wizi."













© Copyright 2005,
Inter Region Economic Network, Nairobi, Kenya, All Rights Reserved.