Chapter 38 - SURA YA THELATHINI NA NANE
TAI, VIBAPARA, WALAGHAI NA WAFALME
Asubuhi iliyofuatia miale ya kwanza ya jua ilimwamsha Jonathan. Alisikia mngurumo mwembamba; Mise alikuwa akifurahia mwayo mrefu -makucha kaiyakita ardhini. Jonathan aliyasugua macho yake na kutizama huku na huku kwa unyonge. Isipokuwa tu mipao michache ya moshi mji ulionekana mtulivu tena. Huku akizongwa na njaa, alichunguza mifukoni mwake akakuta silesi kadhaa za mkate zilizokuwa zimesalia. Alikula moja na , huku akijitahidi kutomwamsha, alitia silesi moja taratibu chini ya mkono wa Alisa. Lakini aligutuka akaketi.
"Ninataka kuangalia juu ya mlima huu," Jonathan alimwambia. Alikubali na pamoja wakaanza kuelekea upande wa juu wa ule mwinuko.Punde si punde waliifikia miamba iliyohitaji msaada wa mikono vile vile na kujivuta kwa kutumia tawi au mzizi wowote uliotokeza.Alikuwa mbele ya Alisa, lakini nyuma ya Mise, Jonathan aliifikia sehemu ya mwamba uliyotokea juu karibu na kilele. Aliukagua mji kwa bali kule chini. Kilele kilikuwa karibu.Hivyo alipanda zaidi kupitia kwenye kichaka cha miti mifupi mifupi iliyojipindapinda.
"Watu !" alijisemea mwenyewe akiwa amekereka . "Wamo katika kusukumana. Wanatishana . Wanakatana. Wananyang'anyana vitu na kuhasimiana."
Hatimaye , miti ilipungua ikiwacha vichaka vichache, na kisha ,rundo, ya mawe makubwa makubwa. Mwezi mzima bado ungeweza kuonekana ukififia kwenye alfajiri,ukiujongelea upeo. Jonathan alihisi hewa ikiwa baridi na ya kuvutia alipokuwa akiendelea kukwea. Kileleni palikuwepo mti mmoja wenye sura mbovu. Juu ya mti hu palikuwepo tai mweusi mwenye sura ya kutisha aliyekuwa katulia kasima kwa mguu mmoja. "Oh, la," alilia Jonathn .Ni nani aliyefarajia kupapata pahali penye upeke zaidi. "Bahati yangu kwa kweli ninaacha nyuma bonde zima la fai ili kuja kupata amani na ninaishia kupata nini? Tai mwenyewe hasa!"
"Mie ni tai mkubwa!" ilisikika sauti nzito na yenye kukwaruza.
Jonathan aliganda. Mise aliruka, kisha akakunja mgongo wake na kuanza kutoa mlio mkali. Macho ya Jonathan, yakiwa yamekuwa makubwa kuliko mwezi, yalizunguka taratibu,yakilikagua lile eneo. Moyo ulisikika ukitandika kwa nguvu masikioni mwake . Huku akitetemeka midomo, aliuliza, "Nani kasema?" Ile sauti ilirudia ilisikika kama iliyotoka kwenye uli mti pweke.
Jonathan alimtizama yule ndege aliyefanana na tai .Hakusogea Jonathan na ndege vile vile. Alisema, "Wewe huongea? La, tai hawaongei!"
Huku akiukusanya ujasiri wake ,Jonathan alikaribia ule mti polepole.Yule ndege hakutikisa hata unyoya, japo alifikiwa hasa kuwa ndege huyo alikuwa akimwangalia muda huo wote.
Jonathan alitamka tena, akijitahidi kuhifadhi sauti yake , "Wewe huongea?"
"Na si ndio ?"alijibu tai kwa kiburi . "Mimi ni tai mkubwa , ndimi mkubwa zaidi katika jamii yenye fahari ya tai." Magoti yake Jonathan yalibonyea ghafla nusura aanguke. Alijigundua na akashuka kuchuchumaa mbele ya ule mti. "Una- unaweza kuongea?"
"Hmm,"alijibu yule ndege. "Nawe waweza? Unaelekea kutofahamu unachosema aghalabu ya wakati. Ninadhani unaiga tu. "Yule ndege aligeuza kichwa chake kidogo na kusema kwa sauti ya tuhuma. "Ulikuwa na maana gani uliposema uliacha bonde zima la tai?"
"Ku-ku-kunradhi. Sikunuia kukutusi ," alikokota Jonathan huku akijihisi mjinga kwa kiasi fulani, kwa jinsi alivyokuwa akizungumza na ndege. "Wale watu wote kule chini walionyesha uhasama na ukatili mwingi miongoni mwao. Ni tamathali ya usemi tu kuwahusu tai na wengineo. Watu hao walinikumbusha, ah, walinikumbusha…."
"Tai?" Yule ndege aliumua manyoya yaliyokuwa chini ya kichwa chake kitupu. Jonathan aligoteza kwa unyenyekevu.
Alisa alichomoza kutoka mitini na yale mazungumzo kati ya Jonathan na tai yalimstaajabisha ghaya ya kustajaabu. "Huwepo!" alimaka. Alichapuka kuelekea alipokuwa Jonathan, Akambana mkono huku akimnong'onezea, "Tai Maarufu Bard kwa hakika huwepo! Nikidhani zilikuwa ngano tu.Sikuwahi kufikiria- tena mkubwa na mwenye sura ya kutisha!"
Tai yule Aliguna na kupiga. Mbawa zake nzito kabla ya kutulia tena kwenye tagaa lake. "Ahsante Alisa kwa kututambulisha ka ukarimu."
Alipoona jinsi Alisa alivyostaajabu kwa kulisikia jina lake, Bard alisema, "Wewe ulinijua kabla. Mbona nami nisiwajue wewe na rafikiyo,Jonathan?"
Alisa na Jonathan walimtizama yule tai kwa hofu kubwa.
"Nimekuwa nikiwatazama nyote wawili kwa muda sasa, na hasa Jonathan katika jaribio lake la harrowing , baharini," akasema Bard. "Ujasiri na mwerevu, kijana,lakini mwepesi wa kupumbaza. Alisa ni mkakamavu zaidi, anayeelekea kuamini matendo zaidi ya maneno."
"Sielewi," akasema Jonathan
"Kwako wewe ,nchi hii yote ni tai tu .Ah! kama ingekuwa hivyo basi hiki kingekuwa kisiwa kizuri zaidi ikilinganishwa na kilivyo sasa." Yule ndege aliinua kichwa chake kitupu,kisichiovutia kwa madaha. "Mmekuja kwenye kisiwa chenye viumbe wengi -tai, vibapara,wezi, na wafalme. Lakini hamtambui ni yupi mwenye kufaa zaidi maana majina na maneno yanawakanganya. Mmekumbwa na ghiliba ya awali kabisa na mnautukuza uovu."
Jonathan alijitetea. "Hapana ghiliba.Tai, vibarapara, na kadhalika, wote wanaeleweka kwa urahisi. Nilikotoka tai huokota mifupa ya wafu. Inaudhi kwa kweli! "Pua ya Jonathan ilikunjana kwa kusisitiza. "Vibapara ni sahili na hawana hatia. Wezi ni waerevu na wacheshi- watundu kwa namna fulani."
"Kwa upande wa wafalme na utukufu." Aliongezea Jonathan haraka,macho yake yakicheza kwa uchangamfu, "Ah ,sijawahi kukutana na yeyote katika maisha halisi ,lakini nimewahi kusoma kuwa wanaishi kwenye maeneo ya kupendeza na kuwaa huvaa mavazi ya kucvutia kweli kweli. Kila mtu hutaka kuwa kama wao. Wafalme na mawaziri wao hutawala nchi na huwa na jukumu la kuwalinda watawaliwa wao wote.Hapo hapana ghiliba."
"Hapana ghiliba?"alirudi bard ,akionyesha uchangamfu. "Hebu mfikirie tai. Miongoni mwa hao wane,ni tai pekee mwenye utukufu wa kweli. Ni tai pekee afanyaye chochote cha muhimu."
Yule ndege mkubwa mweusi alinyosha shingo yake tena na kumkodolea macho Jonathan. "Kila panya ajiapo nyua ya ghala , ninasafisha.Kila farasi ajiapo kondeni, ninasafisha. Kila mkata ajiapo nichakari, ninasafisha. Ninapata mlo na kila mtu ananufaika. Hakuna aliyewahi kubidka kutumia bunduki au mtego ili kunishurutisha kufanya kazi yangu. Na wadhani ninapata shukrani zozote? Hapana ,huduma yangu huchukuliwa kuwa ni chafu na mbaya kwa hivyo sharti mtindiza tai aishi na matusi na bila shukrani yoyote.
"Kisha kuna vibapara," akaendelea tai. "Hawazalishi mali. Hawamfai yeyote isipokuwa wao wenyewe. Lakini hawamdhuru yeyote pia.Wanajilinda dhidi ya kufia vichakani, ama kweli . Na twaweza kusema kuwa wanawafanya wafadhili wajihisi nafuu. Kwa hivyo hukubalika.
"Walaghai ndio wajanja zaidi na wamesifika katika ushairi na ngano. Ni wadanyifu na huwaongopa wengine kwa maneno wanayosuka. Walaghai hawatekelezi huduma yoyote ya maana, isipokuwa kufunza kutoaminika na sanaa ya ufisadi." Huku akiinua kichwa na kutanua mbawa zake kubwa, yule tai alishusha pumzi.Harufu ya nyamafu ilielea kwenye ile hewa ya asubuhi. "Walio chini kabisa ni wale wenye utukufu. Wafalme hawahitaji kuombaomba au kubazazi, japo wao hufanya hivyo mara kwa mara. Kama wanyang'anyi wao huiba mazao ya wengine kwa kutumia nguvu za kikatili walizo nazo. Hawazalishi chochote ,ilhali wanasimama kila kitu. Na wewe msafiri wangu juha., hustahu huu 'utukufu' huku ukimbeza tai? Kama ungeiona sanamu ya zama,"alidai Bard, "ungesema kuwa mfalme alikuwa mtu maarufu kwa sababu jina lake lilichongwa juu yake. Na hata huifikirii kwa vyovyote mizoga yote ambayo tai walihitajika kuondoa wakati wa ijenzi wa sanamu hiyo.
Jonathan alizungumza , "Kweli ,hapo awali baadhi ya wafalme walikuwa nduli. Lakini sasa wapiga kura huwachagua viongozi wao kwenye Baraza la Mabasiri. Wao ni tofauti kwa sababu -naam, kwa sababu huchaguliwa."
Mabasiri waliochaguliwa kuwa tofauti? Ha!" alimaka tai kwa ukali. "Watoto ado hukuzwa kwa ndoto za utukufuna wakuapo, utukufu bado ndio watautarajiao. Mabasiri wenu waliochaguliwa si chochote zaidi ya wafalme -kwa-miaka-minne na wana-wa-wafalme-kwa-miaka-miwili.Kwa kweli,huseta vibapara, walaghai, na utukufu vyote vikichanganyika na kuwa kimoja! Wao huombaomba au kupangia michango na kura; huvisha kyembe cha ukoka na kuongopea kila wapatapo fursa; huzunguka kisiwani kama watawala. Na wakifaulu katika unyonyaji wao, wale miongoni mwetu wanaozalisha kwa kweli na kuhudumu hufaidi kidogo na kidogo zaidi."
Jonathan alibakia kimya . Alitazama tena kule bondeni na kugoteza kichwa kwa kupoteza matumaini. "Ningependa kupaona pahali ambapo mambo ni tofauti na hivyo. Pahali kama hapo paweza kuwapo?"
Huku akiinua mbawa zake kubwa, yule tai alikurupuka kutoka mtini akatua kwa kishindo karibu na Jonathan na Alisa. Waliruka wakarudi nyuma,wkishtushwa na ukubwa wa yule ndege. Bard aliegemea upande wao ,akiwa karibu mara mbili kimo chao, na upanambawa mkubwa ajabu.
"mngeenda kuona pahali ambapo watu wako huru? Ambapo nguvu hutumiwa tu kujilinda Mngependa kuzuru nchi ambako viongozi wanatawaliwa na sheria zile zile zinazowatawala wengine?
"Oh naam!" alisema Jonathan kwa shauku.
Bard aliwatazama wote wawili kwa makini. Macho makubwa ya yule ndege yalikita abisa ndani ya jonathan, yakimsaka dalli za uaminifu. Kisha aliamuru,"Jonathan, panda mgongoni kwangu." Huyo ndege aligeuka kidogo na kushusha ardhini manyoya mapana na magumu ya mkiani.
Utunduizi wake Jonathan uliupika uoga wake . Alikanyaga kwenye kibonde pale mtini na, kwa makini, akajivuta hadi kwenye pengo jororo baina ya mibawa ya yule ndege. Kisha akamwangalia Alisa kwa tarajio.
"Siwezi kuondoka," aliwaambia wote wawili. "Aila yangu inanitafuta. Ningependa kwenda nanyi wakati fulani, lakin sio sasa."
Uso wa Jonathan ulibadilika. Huku akiwa na tabasamu pana, alitania, "bado sijala kile chamchana cha bure."
Punde tu Jonathan alipomzungushia mikono yulendege kwenye shingo yake nene alihisi maumivu kwenye misuli. Yule tai alipiga hatua ndefu ndefu kwa tabu kidogo ardhini. Alihisi mshituko na wakaelea kwenye upepo ilokuwa ukiongezeka. Alipozama nyuma, Jonathan alimwona Alisaakiwapungia huku Mise kasimama miguuni mwake.
Akiabiria futi nyingi juu ya kile kisiwa ,huku upepo ukimpiga mfululizo usoni, Jonathan alijihisi mchangamfu kweli kweli. Isipokuwa kuwakosa marafiki wachache, aliondoka pale kisiwani kwa furaha. Milima ilitoweka chini ya mawingu na tai akafululiza moja kuelekea kwenye miale mikali ya jua lililokuwa likicha. Bahari pana ya mawingu na maji ilitanda mbele na Jonathan alijiuliza, "wapi".
© Copyright 2005,
Inter Region Economic Network, Nairobi, Kenya, All Rights Reserved.