Chapter 39 - SURA YA THELATHINI NA TISA
MGUNDA USO MWENYEWE
Upepo mwepesi kutoka mbele ulimpita Jonathan usoni. Wakati ulitanuka ukawa masaa na mwendo wa mahadhi wa mpao wa yule tai ulimfanya Jonathan asinzie. Aliota. Alikuwa akikimbia kwenye barabara nyembamba huku akifuaatwa na maumbo yaliyokuwa kama vivuli ya walinzi pamoja na mbwa wao. "Simama wewe 'scawalag'- wewe mgeni mpya!"walipiga kelele . Hofu ilimwingia , huku akiendelea kutupa miguu yake kwa nguvu zaidi. Umbo moja lililotokeza mbele ya mengine- Bibie Tweed. Alizisikia pumzi za mwanamama huyo zikiteremka shingoni mwake huku akijitahidi kumbamba kwa vidole vake vinene.
Jonathan aligutushwa na kishindo kikubwa . "Nini? Aliboboa Jonathan akiwa bado ameyashikilia kwa nguvu manyoya azito ya yule ndege.
Walikuwa wametua kwenye ufuo aliodhani aliufahamu. Bard alitoa maagizpo. "Fuata huu uanda kando kando ya bahari .
Uendelee kwa maili moja hivi kuelekea kaskazini na utapata kufahamu ulipo." Vichaka vizito vya nyasi vililikisika pole pole kwenye vilima vya mchanga vyenye rangi ya dhahabu. Bahari ilionekana yenye rangi ya kijivu na baridi pale ilipogusa ufukwe. Alishuka taratibu kutoka mgongoni mwa yule ndege.
Ghafla Jonathan alitamua alikokuwa. "Niko nyumbani!" alipaaza sauti kwa furaha. Alianza kukimbia kwenye miteremko yenye mchanga pale ufuoni kisha akasita ghafla na kumgeukia yule tai. "Lakini , ulisema ulikuwa ukinipelekea pahali ambapo vitu hufanywa ipasavyo." AlisemaJonathan.
"Nimefanya hivyo," alisema Bard.
"Sivyo ilivyo hapa," alibisha Jonathan.
"Labda bado ,lakini itakuwa hivyo ukiiwezesha kuwa hivyo. Popote pale ,hata Corrumpo, paweza kuwa paradiso ikiwa wakaazi wako humu kabisa."
"Corrumpo ?" alishtuka Jonathan . "Wengi wanaamini wako huru vya kutosha. Bibie Tweed aliwaeleza hivyo. Na waliosalia wanauogopa uhuru, na wana shauku kubwa kujitoa kwa Mdadisi Mkuu."
"Maneno matupu!" alisema bard. "Mtihani wa uhuru huja na vitendo." Jonathan alijihisi mtoto sana. Alivuta tete kutoka ardhini na kuanza kudungadunga mchanga huku akiwaza. "mambo yapaswa kuwaje kwani? Nimeona matatizo mengi- lakini masuluhisho ni yepi?"
Tai aliliacha swali la Jonathan kuranda baina yao huku akijipuna manyoya yake kwa mdomo.manyoya yalipokwisha kuwa safi na laini , jitai lilitazama kule baharini huku likisema, "unatafuta maono ya mustakabali?"
"Ninadhani hivyo ." alisema Jonathan.
"Hilo ni tatizo. Watawala daima huwa na maono kisha wakawalazimisha wengine. Kumbuka ,kuwa watewala hawana haki ya kufanya chochote mbacho huna haki ya kufanya wewe mwenyewe. Kama hupaswi kukifanya , basi hupaswi kuwaomba wengine kukufanyia."
"Lakini si maono ni muhimu kwa kukujuza unakoelekea?"
"Kwako mwenyewe lakini si kuwalazimisha wengine." Bard aligeuka kumtizama jonathan tena, huku makucha yake yakishikilia na kukita mchanga. "Katika nchi huru, unatia imani yako kwenye wema na uvumbuzi. Maelfuya viumbe wanaofuatia malengo yao wenyewe, kila mmoja akijitahidi, wataweza kuibua ulimwengu bora zaidi kuliko awezavyo kuwafikiria. Zingatia njia za kuwafikia kwanza, kisha matokeo matukufu yatafuatia. Watu walio huru hupata matatizo wasiyotarajia."
Kwa tashwishi Jonathan alingurua. "Lakini hapana atakayenisikiza."
"Usikizwe au usisikizwe na wengine ,unapata nguvu kwa kusema na kutend. Wale wanaosikiza watapata ujasri kutoka kwako." Jitai liligeuka kutizama baharini huku likijitayarisha kuondoka.
Jonathan alipiga kelele, "Ngoja! Nitaweza kuwaona marafiki zangu tena?"
"Ukisha kutayrisha paradiso yako, nitamleta aje kuiona."
Jonathan alilitizama lile dege likijikusanya na kuutoma mwili walo mkubwa kwenye upepo. Muda mfupi baadaye lilipotelea mawinguni.
Jonatha alianza kutembea. Haukumbuka sana kuhusu kutembea isipokuwa mgegedo wa mara kwa mara wa mchanga chini ya miguu yake na mvuno wa upepo dhidi ya mwili wake. Jonathan alitambua kisia cha mawe mawe ambacho ndicho kilichokuwa hasa cha kuingilia kijijini mwao. Punde si punde, alikuwa akikaribia nyumba na ghala vilivyokuwa kando ya bandari -nyumbani kwao.
Babake Jonathan, mwembamba na mwenye uso wa huzuni, alikuwa kasimama akizungusha kamba kwenye baraza la mbele.
Macho yake yalitanuka alipomwona mwanawe akikaribia. "Jon," babake aliita. "Kijana-Jon, umekuwa wapi?" Huku sauti yake ikivuma, alimpazia sauti mkewe aliyekuwa kajishughulisha ndani kusafisha. "Rita tizama, Jon amerejea!"
"Kelele zote hizo ni za nini?"Liuliza mamake Jonathan akionekana mwenye wasiwasi kidogo zaidi ya vile alivyokumbuka. Alitoka akaja barazani na mujarabu wa kumwona mwanawe akipiga usiahi kwa shanwe. Ghafla alimkusanya Jonathan mikononi mwake na kumkumbatia kwa muda mrefu. Kisha akimsukuma nyuma na kumtizama kwa umbali wa mkono alipisha mkono wa nguo yake kwenye macho yake ili kufuta bubujiko la machozi ya furaha. "Kusema kweli umekuwa wapi wewe kijana?Waumwa nanjaa? "Kisha , kwa uchangamfu, alimwambia mumewe, "washa moto , Hubert , na utie buli!"
Wote walisherehekea kwa shangwe kuungana kwao tena, na Jonathan alisimulia aliyoyaona. Wakati mwengine alichora picha sahili kuyafafanua wazazi wake walitabasamu na kutikisa vichwa vyao kutokana na kuamini na furaha. Baada ya kula silesi moja ya mwisho ya kitumbua fufutende cha mamake ,alishusha pumzi na kuegemea kiti chake. Lile ghala zee na sebule yao kwenye chumba cha nyuma viling'aa kwenye mwanga wa jiko. "Mwanangu unaonekana mkomavu," alisema babake. Alimkazia Jonathan macho, na kuongezea kwa mzaha, "Utaabiri tena hivi punde?"
"La, Baba, "akasema Jonathan. "Nipo papo hapa . Kuna kazi nyingi ya kufanya."
© Copyright 2005,
Inter Region Economic Network, Nairobi, Kenya, All Rights Reserved.