Inter Region Economic Network, Nairobi, Kenya  

Home
About IREN
Media & Press
Projects
News & Newsletters
Articles
Events
Resources
Speeches and Publications
Student Outreach
Contact IREN

KIMALIZIO



Bwana Gullible ,mume mwenye busara na ambaye alikuwa mkubwa wangu kwa miaka mingi, alinipa hadithi ambayo ni zaidi ya jasira. Kwa muda wa miezi mingi tuliyowasiliana naye alinipa vidokezo kuhusu falsafa yake inayovutia kuhusu maisha. Kwa miaka mingi falsafa hii ilimwongoza katiaka ufanisi katika shughuli alizozifanya kwao. Hiyo ni hadithi nyingine. Haidhuru, nakuachia maneno kutokana na hitimisho la jarida lake:

Falsafa yangu imejikita kwenye imani ya kujimiliki. Unamiliki maisha yako. Kukana hili ni kumaanisha kuwa mtu mwingine anayo haki kubwa ya kudai maisha yako kuliko wewe mwenyewe. Hapana mtu mwingine au kundi la watu ambalo humiliki maisha yako nawe kadhalika humiliki maisha yao.

Wewe huishi kiwakati: ujao, uliopo, na uliopita. Hili linadhihirishwa katika maisha , uhuru, na zao la aisha yako na uuru. Shughuli ya uteuzi kuhusu maisha na uhuru ni fanaka yako. Kupoteza maisha yako ni kupoteza mustakabali wako. Kupoteza uhuru wako ni kupoteza hali yako ya sasa. Na kupoteza zao la maisha yako pamoja na uhuru ni kupoteza lile mego la misha yako yaliyopita lililolizalisha.

Zao la maisha yako pamoja na uhuru ni mali yako. Mali ni matunda ya kazi yako, zao la wakati wako, nguvu , na talanta. Ni ule mgao wa kimaumbile unaoutumikiza vema. Na ni mali ya wengine mayo hupawa kwako kwa kuadilishana kwa hiari na akubaliano ya pande zote. Watu wawili wanaobadilisha mali kwa hiari wako vizuri la sivyo wasingefanya hivyo.Ni wao pekee wawezao kufanya uamuzi wao vema zaidi.

Wakati fulani watu hutumia nguvu au udanganyifu ili kupata vitu kutoka kwa wengine bila makubaliano ya uchaguo na hiari. Kihali halisi,juhudi za kutumia nguvu kunyakua maisha ni mauaji, kunyakua uhuru ni utumwa , na kunyakua mali ni wizi. Hali hizi ni sawa bila kujali kama mtenda ni mtu mmoja ,wengi wakiwatendea wachache, au hata na maafisa wenye kofia nzuri na wene vyeo.

Unayo haki ya kulinda maisha yako, uhuru na uthibitishe kuwa ya haki mali yako dhidi ya wanyakuzi wengine watakao kutumia nguvu. Hivi utakuwa na haki kuwaomba wenzako wasaidie kukulinda. Lakini huna haki ya kuanzisha matendo ya maguvu dhidi ya maisha, uhuru ,au mali ya wengine. Yaani,huna haki ya kumkodisha mtu ili kuwatumiliza nguvu watu wengine kwa niaba yako.

Unayo haki ya kutafuta viongozi, lakini huna haki ya kuwalazimisha wengine viongozi. Bila kujali kama maafisaa huchguliwa vipi, wao ni binadamu na hawana haki au madai ambayo ni zaidi ya yale ya watu wengine. Bila kuali vyeo vyao vya ubunifu kitabia au idadi ya watu inavyowashabikia, maafisa hawana haki ya kuua, kuwa na watumwa , au kuiba. Huwezi kuwapa haki zozote ambazo wewe huna.

Kwa kuwa unayamiliki maisha yako , unawajibikia. Wewe hukukodisha maisha yako kutoka kwa wengine ambao watakutaka uwe mnyenyekevu. Na wala wewe si mtumwa wa wengine ambao watataka kafarakutoka kwako. Unateua malengo yako kutegemea na thamani yako. Ufanisi na ukosefu ni vivitio muhimu kwa ujifunzaji na ukuaji. Matendo yako kwa niaba ya wengine, au matendo yao kwa niaba yako, yanakuwa yenye wema pale ambapo yanatokamana na kujitolea na makubaliano ya pande zote. Hii ni kwa sabau wema waweza kudumishwa t pale palipo na uteuzi wa hiari.

Huu ndio msingi wa jamii iliyo huria hasa. Mali na ukweli kwamba huu ndio msingi wa kimatendo zaidi na wenye utu kwa matendo ya binadamu, pia ni wenye maadili zaidi.

Matatizo yanayotokana na uanzishwaji wa maguvu na serikali yana tatuzi. Tatuzi ni kwa watu wa ulimwenguni kote kugoma kuwaomba maafisa kuanzisha maumizi ya nguvu kwa niaba yao. Uovu hautokani tu na watu waovu, lakini pia kutoka kwa watu wema ambao hukbali uanzishwaji wa maguvu kama mbinu ya kuwatimilizia haja zao. Kwa jinsi hii, watu wema wamewezesha kuwepo uovu katika vipindi vyote vya historia.

Kuwa na imani katika jamii iliyo huria ni kulenga kwenye harakati ya ugunduzi sokoni penye maadili na wala si kulenga kwenye maono au malego ya lazima. Kutumia uwezo wa serikali ili kulazimisha watu wengine maono ni uzembe wa kiakali na matokeo yake hasa huwa ni kinyume kisichotarajiwa na cha kupotosha. Ili kuweza kupata jamii huria lazima pawe na ukakamavu wa kuwaza, kuzungumza , na kutenda -hasa inapokuwa kwamba ni rahisi kutokufanya cho chote.

Jonathan Gullible






















© Copyright 2005,
Inter Region Economic Network, Nairobi, Kenya, All Rights Reserved.