Chapter 2 - SURA YA PILI
WASUMBUAJI
Jonathan alitembea kwa masaa kadhaa bila kuona ishara yo yote ya viumbe wenye uhai. Mara, kitu fulani kikasikika kikitembea msituni na kisha mnyama mdogo mwenye mkia uliokuwa na milia ya manjano akaonekana. "Paka", alifikiri Jonathan. "Labda atanionyesha kule walioko viumbe wengine wenye uhai." Aliteremka kupitia kwa matawi mengi ya miti ya kisiwa hiki.
Wakati ambapo upeo wake wa macho haungeweza kuona tena ufuo wa bahari kwa kuzama kabisa msituni, ulisikia mlio mkali. Alisangaa, akainua kichwa chake, na akajaribu kuona kama sauti hiyo ilikuwa imetokea wapi. Mkabala naye, alisikia sauti nyingine kali ikiomba usaidizi. Kwa kujisukumiza mbele kupitia kwenye matawi mengi na mizabibu alipata njia iliyompa kupata njia kubwa zaidi.
Alipoizunguka kona kali pale njiani, Jonathan alikumbana na bandikizi la mume. "Niondokee, kijitu wee!" alikemewa na yule mwanamume, huku akimsukuma kando kana kwamba ni mbu mdogo. Akiwa amechanganyikiwa, Jonathan aliinua macho yake na kuona waume wawili wakiwa wanamburura njiani msichana mmoja aliyekuwa akipiga mateke huku akilia. Kufikia wakati ambapo alizindukana, wale watu watatu walikuwa wametokomea. Huku akiwa ametambua kuwa yeye pekee hangeweza kumwokoa yule mama, Jonathan alikimbia barabarani akitafuta usaidizi.
Alifika mahai penye weu na ambapo aliona kundi la watu wakiwa wameuzunguka mti - wakiupiga kwa vijiti. Jonathan alifiatuka mbio na kuushika mkono wa mme mmoja ambaye ndiye aliyeonekana kama kiongozi. "Tafadhali bwana, saidia!."
"Usifanye wasiwasi', alijibu yule bwana kijeuri. "Ameshikwa. Achana naye na uendelee na shughuli zako, sisi tunayo kazi ya kufanya." "Kushikwa?" Jonathan alishangaa ni kwa nini mama huyu aliomba msaada kwa kulia jinsi alivyolia kama alikuwa na hatia. "Naomba samahani, bwana, lakini kosa lake ni lipi?" "Huh?" alijibu yule bwana kwa hasira. "Naam, kama ni lazima ujue, alihatarisha kazi za sisi sote tunaofanya kazi hapa."
"Eti alihatarisha kazi za watu? Je, angewezaje kufanya hilo?" aliuliza Jonathan.
Kwa kumwangalia msaili wake mjinga kutoka juu, kiongozi huyu alimwambia Jonathan aandamane naye hadi pale mtini ambapo wafanyakazi walitwanga shinani pa mti kwa bidii. Kwa majivuno alisema "Sisi ni wafanyakazi tunaoshughulika na miti. Huwa tunaiangusha miti kwa ajili ya mbao kwa kuitwanga na vijiti hivi. Kuna wakati ambapo watu mia, wafanyapo kazi usiku na mchana, waweza kuangusha mti wenye ukubwa kiasi kwa muda unaopungua mwezi." Mume huyu aliikunja midomo yake na kisha akajipanguza taratibu kipande cha uchafu kutoka kwa mikono ya koti lake lililotengenezwa vema.
Kisha akaendelea, "Yule mwanamke Drawbaugh alikuja kazini asubuhi ya leo akiwa ameambatisha kifaa kali cha chuma kwenye ncha ya kijiti chake. Aliweza kuukata na kuangusha mti kwa muda usio saa moja yeye peke yake! Fikiria hilo! Tendo baya kama hili na ambalo linatishia shughuli yetu ya toka jadi lilifaa kukomeshwa."
Jonathan alifumbua macho, akashangaa kusikia kuwa mama huyu aliathibiwa kwa kuwa mbunifu. Nyumbani kwao kila mtu alitumia shoka na misumeno kwa kuikata miti. Hivyo ndivyo alivyozipata mbao za kutengeneza mashua yake. "Mbona ubunifu wake, " alishangaa Jonathan, "Ubunifu huwawezesha watu wa vimo na nguvu tofauti tofauti kuikata miti. Je, si hali hii huharakisha na kurahisisha upatikanaji wa mbao?"
"Una maana gani?" Yule mwanamume aliuliza kwa hasira. "Mtu atawezaje kuruhusu wazo kama hilo? Hii kazi mufti haiwezi kufanywa na mnyonge ye yote ambaye atajitokeza na wazo jipya."
Huku Jonathan akijaribu kutomwudhi bwana huyu alisema, "Lakini bwana, si hawa wafanyakazi wazuri wa mtini wana mikono mielekevu pamoja na akili. Wanaweza kuutumia muda utakaosalia kutokana na wao kutotumia vijiti kuangusha miti kufanya mambo mengine. Wanaweza kutengeneza meza, kabati, mashua, au hata nyumba!"
"Sikiza, wewe," alisema yule bwana kwa mwangilio wa kuogofya, "lengo la kazi ni kumshughulisha mtu kila wakati pasi na kuwa na wasiwasi wa kuimaliza - siyo kujitokeza na mazao mapya." Toni ya sauti yake ilisinya. Unaonekana msumbuaji. Yeyote amwungaye mkono yule mke mbaya sana ni msumbuaji. Je, wewe watoka wapi?"
Jonathan alijibu kwa hofu, "Mimi simjui Bi.Drawbaugh na sina nia ya kuwa msumbufu, bwana. Nina imani hukukosea. Naam, naomba kuondoka." Baada ya kuyasema hayo, Jonathan alipinduka ili kurudi kule alikokuwa ametoka, huku akitelemka njiani harakaharaka. Kukutana kwake kwa mara ya kwanza na watu wa kisiwa hiki kulimwogofia.
© Copyright 2005,
Inter Region Economic Network, Nairobi, Kenya, All Rights Reserved.