Inter Region Economic Network, Nairobi, Kenya  

Home
About IREN
Media & Press
Projects
News & Newsletters
Articles
Events
Resources
Speeches and Publications
Student Outreach
Contact IREN

Chapter 3 - SURA YA TATU


Tanzia ya Makabwela

Njia ilipanuka kidogo kadiri ilivyopita kwenye msitu huo mzito. Jua lililokuwa mti-kati lilikuwa kali na lilichoma Jonathan kwenye kipaji chake kabla hajapata ziwa dogo. Alipochota maji ili aweze kujiburudisha kwayo, Jonathan aliisikia sauti ya mtu fulani ikimpa onyo, "Lau kama ningekuwa wewe nisingeyanywa hayo maji."

Jonathan alipotupa jicho huko na huko alimwona mzee wa kiume akiwa amepiga magoti kwenye ukingo wa bahari, akiwa yuaosha samaki wachache wadogo kwenye ubao. Kando yake kulikuwa na ndoo, kijiti cha kukunjia nyuzi, na fito tatu zilizokuwa zimehimiliwa kwenye udongo, kila mojawapo ikiwa imening'inizwa majini uzi wa kuvulia. "Je, uvuvi ni mzuri?" alisaili Jonathan kwa upole.

Bila kujali kama aliyeuliza alikuwa wapi, yule bwana alijibu kwa utundu fulani, "Hapana. Hivi visamaki vidogo pekee ndivyo nilivyopata leo." Aliendelea kutengeneza nofu za samaki huku akizitupa kwenye chungu moto uliokuwa ukiwaka bila ulimi wake. Samaki zilizochachatika kwenye sufuria zilinukia vema. Jonathan aliweza kumwona yule paka sungu aliyekuwa na milia ya manjano na ambaye alikuwa amemfuata huku akiwa yuala masalio ya samaki. Alitamani sana zile samaki.

Jonathan, ambaye alijidhani kuwa ni mvuvi stadi, alijiuliza, "Je ni nini ulichokitumia kama chambo?"

Yule mume alimwangalia Jonathan huku akiwaza "Hamna chochote kibaya na chambo zangu, kijana. Nimenasa kilicho chema katika kile kilichokuwa kimesalia ziwani hapa."

Jonathan aligundua hali ya upweke katika yule mvuvi na kwa hivyo akadhani kwamba kwa kuwa mnyamavu kidogo, angeweza kujifunza mengi kutoka kwake. Hatimaye, yule mzee mvuvi alimwomba kwa kumkonyezea mkono aketi kando ya moto ili wale pamoja baadhi ya zile samaki na kipande cha mkate. Jonathan alikila chakula chake kama mwenye njaa kubwa, japo alihisi kuwa yuamkosea yule mvuvi kwa kule mego la mankuli yake madogo ya mchana. Walipomaliza kula, Jonathan alikaa kimya na hapo ndipo yule mzee alianza kuzungumza. "Miaka ya zamani kulikuwa na samaki wakubwa ambao wangeweza kuvuliwa hapa" yule bwana alisema huku akionyesha ishara ya kuwa na mengi. "Lakini wote wamevuliwa. Sasa hivi waliosalia ni wadogo tu."

"Ila hawa wadogo watakua, au siyo?" Jonathan aliuliza. Aliyakodolea macho manyasi yenye majimaji yaliyokua kwenye ukingo wa ziwa wenye maji haba ambapo pana uwezekano wa samaki wengi kujificha.

"Ah. Watu wavua samaki wote, hata wale wadogo. Na si hayo tu, watu wanatupa taka kikomo cha ziwa. Lione lile rundo la taka ule upande mwingine?" Jonathan alionekana aliyeshangazwa. "Mbona watu wengine waja kuwachukua samaki wenu na kisha wanatupa taka ndani ya ziwa lenu?"

"Ah, hapana," alisema mvuvi, "hili si ziwa langu. Ni miliki ya kila mtu - ni kama vile misitu na vijito."

"Hawa samaki ni miliki ya kila mtu ….." Jonathan alisita, "hata mimi?" Hapa ndipo ile fikira ya kukosa kwa kula chakula ambacho hakushiriki kukitayarisha ilianza kumtoka.

"Si hivyo hasa", yule bwana alijibu. "Kile kilicho cha kila mtu si cha ye yote - yaani, mpaka samaki akamatwe na ndoana yangu. Hapa ndipo anapokuwa wangu."

"Sielewi," alisema Jonathan, huku akiwa amekunjamana uso ishara ya kuchanganyikiwa. Huku akiwa kama anayejiongelesha nusu bin nusu, alikariri tena, "Samaki ni miliki ya kila mtu, imaanishayo kuwa si miliki ya ye yote, mpaka pale anapouma ndoana yako. Hivyo basi, samaki ni wako? Lakini je, kunalo lo lote ulifanyalo ili kuwatunza samaki hawa au kuwasaidia kukua?"

"Bila shaka, la" yule mume alisema kwa mkoromo wa madharau. "Mbona niwajali samaki ambao ye yote anaweza kuja hapa wakati wo wote na kuwavua? Endapo mtu mwingine atawavua hawa samaki au atachafua ziwa hili na taka, juhudi zangu zitakuwa zimeambulia patupu!"

Kwa mtazamo wa maji yale ulioonyesha huzuni, yule mvuvi mzee alisema kwa sauti ya majonzi, "Natamani sana kuwa mwenye kumiliki ziwa hili. Hivyo ningehakikisha kuwa samaki wametunzwa vema. Ningetunza ziwa hili jinsi afanyavyo mtunza - mifugo anayesimamia uwanda na kufugia mifugo pale penye bonde lile jingine. Ningezalisha samaki thabiti zaidi, wanono zaidi na amini usiamini singeruhusu wezi wa samaki au watupa taka. Ningehakikisha kuwa....."

"Ni nani anayesimamia ziwa hili sasa?" Aliingilia kati Jonathan.

Uso ulionyauka wa mvuvi ulionyesha kuwa ni mwenye sura mbaya. "Ziwa hili laendeshwa na Baraza la Watawala: Kila baada ya miaka minne, Watawala wachaguliwa kujiunga na Baraza. Halafu Baraza huteua meneja ambaye hulipwa kutokana na ushuru mwingi wa Baraza. Meneja wa samaki anahitajika kuhakikisha kuwa uvuvi haufanywi sana na kuwa taka hazitupwi ziwani. La kushangaza ni kuwa marafiki za Watawala huvua samaki na kutupa taka ziwani jinsi wapendavyo."

Wote wawili walibarizi huku wakiuona upepo ukifanya ruwaza ya viwimbi upande wa pili wa lile ziwa la fedha. Jonathan aligundua kuwa kulikuwa na yule paka wa kimanjano akiwa kaketi kiwimawima, avuta harufu puani, huku akiwa kakodolea macho kichwa cha samaki kilichokuwa kwenye sahani yake. Alimtupia kichwa cha samaki naye paka akakidaka vema kwa guu moja lenye kupindika. Paka huyu alionekana shupavu, na alikuwa na sikio lililoraruka kutokana na vita fulani aliyopigana zamani.
Huku akifikiria kisa cha huyu mvuvi mzee, Jonathan aliuliza, "Je ziwa hili husimamiwa vema?"

"Jionee mwenyewe", yule mzee mvuvi alinung'unika. "Tazama kiasi kidogo cha mawindo yangu. Yamkinika samaki hupungua kwa ukubwa kadiri mshahara wa meneja unavyozidi kuwa mkubwa."








© Copyright 2005,
Inter Region Economic Network, Nairobi, Kenya, All Rights Reserved.