Inter Region Economic Network, Nairobi, Kenya  

Home
About IREN
Media & Press
Projects
News & Newsletters
Articles
Events
Resources
Speeches and Publications
Student Outreach
Contact IREN

Chapter 4 - SURA YA NNE


MAPOLISI WA VYAKULA

Vijia vilikutanishwa na maburuzo ya taka yaliyopanuka na kuingia kwenye barabara ya mashambani yenye changarawe. Badala ya kupitia msituni, Jonathan alikumbana na manyasi yaliyofingirika ya malisho kwa mifugo pamoja na mashamba ya mazao yaliyoelekea kukomaa, na mashamba yaliyostawi ya matunda. Kule kuona chakula chote hicho kikiwa chakua kulimkumbusha Jonathan kuwa alikuwa amekula chakula kidogo sana wakati wa mankuli ya mchana. Alizunguka kuelekea nyumba safi ya mashambani, huku akitegemea kugundua kama alikuwa wapi na labda kupata chakula kingine.

Alipofika mbele ya baraza ya nyumba hiyo, alimkuta mwanamke wa makamo pamoja na kijana mdogo wa kiume wakiwa wamejikunyata pamoja wakilia. wakilia. "Tafadhalini", Jonathan alisema kijinga. "Je, kuna taabu yo yote?"

Yule mama alitazama juu, huku macho yake yakiwa yameloa kwa machozi. "Ni mume wangu. Ah, mume wangu!" aliangua kilio. "Nilijua kuwa siku moja mambo yatakuja kuwa hivi. Ameshikwa", alilia, "na Mapolisi wa Vyakula?!"

"Nasikitika sana kuyasikia hayo, maama. Je, ulisema Mapolisi wa Vyakula!" aliuliza Jonathan. Alikipapasa kichwa cheusi cha yule kijana kwa huruma." "Mbona wakamshika?"

Yule mama aliyakereza meno yake, huku akijaribu kujizuia asidondokwe na machozi. Kwa bezo, alisema, "Hatia yake ni ile ya kukuza chakula kingi zaidi!"

Jonathan alishangazwa. Kisiwa hiki kilikuwa hasa ni mahali pa ajabu! "Ati ni hatia kukuza chakula kingi zaidi?"

Mama yule aliendelea kusimulia, "Mwaka jana Mapolisi wa Vyakula walitoa amri wakimwambia ni chakula kiasi gani ambacho alifaa kuzalisha na kuuzia wananchi. Walitueleza kuwa bei za chini ziliwaumiza wakulima wengine." Alijiuma kidogo mdomo wake, kisha aka-foka, "Mume wangu alikuwa mkulima mzuri zaidi ya wote wakiwekwa pamoja!"

Ghafula Jonathan alisikia mngurumo mkali wa kicheko ukitokea nyuma yake. Mwanamume mkubwa alitembea kwa madaha toka barabarani kuelekea hii nyumba ya shambani. "Ha!" alicheka kidharau, "Kwangu mkulima mzuri zaidi ni yule anayejinyakulia shamba. Au siyo?" Kwa ishara ya mkono wake mkubwa, yule mume alimgodolea macho yule mama na mwanawe na kisha akatoa amri, "Fungasheni virago vyenu mpaondoke hapa. Baraza la Watawala limenipa ardhi hii."

Yule mume alinyakua kijibwa cha kuchezea watoto kilichokuwa kwenye vipandio na kukitupa mikononi mwa Jonathan. "Nina uhakika anaweza kuwa na umuhimu kwako, kijana. Harakisheni, hapa mahali sasa ni pangu."

Yule mama alisimama, macho yake yakiwa yamefumbikwa kwa hasira, "Wewe huwezi kuwa mkulima mzuri jinsi mume wangu alivyokuwa."

"Hili ni suala la mjadala", yule mume alijichekea kwa kiburi. "Ndio, alikuwa na mapenzi kwa kilimo. Pia alijua kwa yakini kama apande nini na jinsi ya kuwapendeza wateja wake. Alikuwa ni mume hasa! Lakini alisahau kitu kimoja ------ Baraza la Watawala ndilo liwekalo bei na vyakula vya kupandwa. Nao wana Polisi wa Vyakula ndio wanaotilia nguvu sheria za Baraza la Watawala."

"Vimelea nyingi!" alipiga kelele yule mama. "Kila mfanyalo haliwi, mnaharibu mbolea na mbegu nzuri kwa cho chote mpandacho, na hapana atakaye kununua kile mpandacho. Mnapanda kwenye ardhi tambarare iliyo na mafuriko ya maji au kwenye udongo mzito uliokauka na hamjali kama mtapoteza kila kitu. Mnaliachia tu Baraza la Watawala kulipia uozo huo. Wameweza hata kukulipeni kuharibu mazao yote."

Jonathan alikunja uso kwa masikitiko, "Kwani kuwa mkulima mzuri hakuna faida?"
"Kuwa mkulima mzuri ni kizuizi" alijibu yule mama huku uso wake ukionyesha hasira. " Mume wangu, kinyume na mjipendekeza huyu, alikataa kuwadanganya wana Baraza la Watawala na akajaribu kuzalisha mazao ya kweli yaliyouza kweli."

Huku akimsukuma yule mama na mtoto wake kutoka kwenye baraza ya kuingilia nyumbani, yule bwana alinguruma, "Tosha! Alikataa kufuata mikidari za kila mwaka. Yeyote apingaye Mapolisi wa Vyakula sharti ajute. Sasa iondokee ardhi yangu!"

Jonathan alimsaidia mama yule kubeba vikorokoro vyake. Mama huyu na mwanaye walitembea pole pole kutoka kule kulikokuwa nyumbani kwao. Walipofika kona moja kule barabarani, wote waligeuka ili waweze kuona kwa mara ya mwisho nyumba safi na ghala la nafaka. "Ni nini kitachotendeka kwako sasa?" Jonathan aliuliza.

Mama yule alihema, "Siwezi kumudu gharama ghali ya vyakula. Kwa bahati, tunao jamaa na marafiki tunaoweza kuwategemea. La sivyo, ningeliomba Baraza la Watawala kunitunza mimi pamoja na Daudi. Hilo wangelikubali", alisema kimbubujiko na kwa ukali. Kwa kumshika mtoto wake mkono na kulichukua furushi kubwa, alisema "Njoo twende, Daudi."

Jonathan alijishika tumbo ---- wakati huu alikuwa akihisi kuwa alikuwa mgonjwa zaidi kuliko alivyohisi njaa.





© Copyright 2005,
Inter Region Economic Network, Nairobi, Kenya, All Rights Reserved.